Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala: Bamako wanakufa kwa Mkapa

MAYELE BANGALA.jpeg Straika Yanga mambo magumu Championship

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Yanga,Yannick Bangala amesema kuwa kwa hali yoyote ile lazima wahakikishe wanapata ushindi katika mchezo wao ujao wa kimataifa dhidi ya Real Bamako.

Yanga wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Real Bamako katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo Jumatano katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa wa pili kwenye msimamo wa Kundi D la michuano hiyo wakiwa na pointi nne nyuma ya US Monastir wenye saba.

Bangala alisema: “Unajua kwa sasa sisi wachezaji tunahitaji kucheza robo fainali na wala siyo hatua yoyote ile nyingine. Malengo yetu makubwa ni kuhakikisha kuwa tunafika huko na kama tunahitaji kufika huko lazima tutumie vizuri uwanja wetu wa nyumbani kwa kuhakikisha tunashinda dhidi ya Real Bamako kisha kushinda tena dhidi ya US Monastir.

“Najua ni kazi ngumu lakini wachezaji tumeongea na tumejipanga kufa na kupona uwanjani ili tuweze kushinda michezo yetu hiyo miwili muhimu, lakini huu wa kwanza dhidi ya Real Bamako ni muhimu zaidi kwetu kupata matokeo, tukishinda tutakuwa na amani kubwa ya kupambana katika michezo miwili iliyobaki,” alisema mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: