Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bamako watua Bongo na jina la Mayele

Fiston Mayele Tetema Bamako watua Bongo na jina la Mayele

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kuelekea mchezo wao wa kesho Jumatano dhidi ya Yanga, kikosi cha Real Bamako tayari kimewasili nchini usiku wa kuamkia juzi Jumapili huku wakichimba mkwara mzito kuwa wamekuja kusaka pointi tatu dhidi ya Yanga.

Yanga kesho Jumatano wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Real Bamako katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Huu unakuwa mchezo wa nne kwa timu zote mbili katika hatua hiyo ya makundi huku pia ukiwa mchezo wa marudiano baada ya timu hizo kukutana Jumapili iliyopita kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa nchini Mali na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo bao la Yanga lilifungwa na straika Fiston Mayele.

Matokeo hayo yaliifanya Yanga kusalia katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi D la mashindano hayo baada ya kufikisha pointi nne huku Real Bamako wao wakisalia kwenye nafasi ya mwisho na pointi zao mbili walizokusanya kwenye michezo minne.

Akizungumza nasiu, golikipa wa Real Bamako, Bourama Togola alisema: “Tunafahamu kuwa utakuwa mchezo mgumu kwetu, Yanga wana kikosi kizuri tuliwaona kwenye mchezo wetu wa kwanza, lakini hii ni nafasi nyingine kwetu na tuko hapa kuhakikisha tunapambana kupata pointi tatu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: