Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke: Kazi imeanza, nitawafunga sana!

Baleke Hjks Baleke

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupachika mabao matatu ‘Hat trick’ kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar jumamosi iliyopita, mshambuliaji wa Simba, Mkongomani Jean Baleke amefunguka sasa kutaka kufunga zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba ipo nafasi ya pili ya Kundi C.

Mabao hayo matatu aliyoyafunga ndani ya dakika 31 yalimaliza mechi hiyo kwani ndiyo pekee yaliyopatikana na mchezo kumalizika kwa Simba kushinda 3-0 ikikusanya alama tatu na kufikisha pointi 57 ikisalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Akizungumza nasi, Baleke aliyesajiliwa na vigogo hao wa Msimbazi kwenye dirisha dogo lililofungwa mwezi Januari akitokea TP Mazembe amesema amefurahishwa na Hat trick ile na sasa anajipanga kufanya makubwa zaidi katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya.

Aidha Straika huyo mwenye mabao matano hadi sasa kwenye ligi ameweka wazi sababu za kukosa muendelezo wa kufunga katika mechi zilizopita akiutaja ugeni na kutopata muda wa kutosha kucheza kuwa kikwazo kwake.

“Nimefurahi kufunga na kuipatia timu yangu ushindi, haya mabao yameniongezea morali na hali ya kujiamini zaidi na nataka niendelee klufanya hivi kwenye kila mechi,” alisema Baleke nas kuongezaa;

“Awali sikuwa na muendelezo mzuri wa kufunga lakini sababu kubwa ni uzoefu, nimeingia kwenye timu katika dirisha dogo hivyo nilihitaji muda wa kuzoeana na kujua timu inachezaje kiujumla na sasa angalau tumezoeana na naamini tutafanya makubwa zaidi,” alisema Baleke.

Nyota huyo pia amemtaja mshambuliaji wa Yanga kama moja ya mastaa wanaoweza kuwa vinara wa mabao msimu huu kutokana na kuongoza hado sasa akiwa amefunga 15 huku Baleke yeye akitaka walau 10 tu.

“Kwa sasa na mechi zilizobaki ni ngumu kwangu kuwa mfungaji bora, kuna wachezaji wenye mabao mengi kama Mayele, Saido na Phiri, nadhani hao wana nafasi kubwa ya kufanya hivyo,”alisema Baleke na kuongeza;

“Mayele namjua kwani nikiwa Mazembe alikuwa vita na tulikuwa na ushindani mkubwa, lakini kwa sasa ninachokifanya ni kuhakikisha naisaidia timu kupata ushindi na kama kufunga basi hata nikimaliza msimu na mabao 10 sio mbaya kwani nimekuja katikati.”

Ikumbukwe misimu miweli nyuma wakati Baleke yupo Mazembe aliibuka mfungaji bora wa ligi ya DR Congo ‘Linafoot’ akiwa na mabao 14 na nyuma yake alifuatiwa na Mayele aliyekuwa AS Vita na mabao 13 na msimu uliofuata alisajiliwa na Yanga.

Simba kwac sasa inajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Horoya kutoka Guinea itakayopigwa Machi 18, mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni marudiano baada ya Wenkundu wa msimbazi kupoteza kwa kuchapwa 1-0 ugenini.

Kama Simba itashinda mechi hiyo, itakuwa imekata tiketi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu kwani itafikisha alama tisa kwenye kundi B ambazo tofauti na Raja Casablanca inayoongoza kundi na pointi 12 hakuna timu nyingine kati ya Horoya na Vipers itakayoweza kuzifikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: