Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kumkosa Chivaviro, Orlando nao wamgeukia Mayele

Mayele Yanga Chivaviro Baada ya kumkosa Chivaviro, Orlando wamgeukia Mayele

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Club ya Orlando pirates kutoka Afrika Kusini baada ya kukosa Saini ya Mshambuliaji hatari kutoka Malumo Gallants, Ranga Chivaviro aliyejiunga na Amakhosi majina yafuatayo wanayo mezani ili kutibu gonjwa la eneo lao la mshambuliaji wa kati.

GUY MBENZA[23]

Mshambuliaji wa kamataifa wa Congo Brazaville [Zaire] anayekipiga ndani ya kikosi cha Al-Tai inayoshiriki ligi kuu ya Saudia (Saudia Pro League) yupo katika rada za Orlando pirates kutoka Afrika Kusini wakiamini uwezo wake na uzoefu wake ndani ya ligi ya Afrika unaweza kuwasaidia wakati huu wanaporejea kimataifa msimu ujao.

FISTON KALALA MAYELE[29]

Mshambuliaji wa kimataifa wa DRC na klabu ya Yanga Sc Mayele. Yupo katika karatasi za Orlando Pirates ambao wanaona Mayele ni mtu sahihi kwao kwa kazi kubwa aliyoifanya msimu ulioisha akiwa na mafanikio mengi sana yeye kama yeye na klabu kwa ujumla.

ASHLEY CUPIDO[22]

Mshambuliaji wa Cape Town Spurs iliyopanda daraja nchini Afrika Kusini naye ni miongoni mwa majina yaliyopo kwenye note book ya Orlando pirates.

Huyu ndiye kinara wa mabao katika ligi daraja la kwanza nchini Africa kusini msimu ulioisha na anatajwa kama mchezaji bora anayechipukia atayekuja kulisaidia taifa la Afrika Kusini.

BENSON OMALA[21]

Kinara wa mabao na mshambuliaji wa Gor Mahia naye anatajwa kuwaniwa na klabu ya Orlando Pirates. Amemaliza ligi akiwa na mabao 26 nyuma ya top scorer Elvis Rupia kutoka Police FC aliyefunga mabao 28.

ETIOSA IGHODARO[24]

Mshambuliaji wa Chippa United aliyekuwa miongoni mwa wachezaji 6 waliofunga magoli 10 na kuendelea nae yupo kwenye rada za Pirates na inasemekana huyu tayari wangeshamsaini ila yupo pale kwa mkopo kutoka Sundowns nao hawapo tayari kumuuza kwa wapinzania wao ugumu ndio upo apo na wanasema watamuuza ulaya sio kwa Pirates hata waje na kiasi gani.

SEDE JUNIOR DION[29]

Mchezaji wa Zamani wa Marumo na Jwaneng Gallaxy anayekipiga kunako Klabu ya Amazulu ni mmoja wa malengo ya Orlando pamoja na timu yake kua na msimu mbovu ila aliweza kufunga mabao 5.

Pirates wamekua wakiulizwa kwa nini mtasaka kwa nguvu mshambuliaji na malengo yapo kwa wachezaji wengi. Jibu lao limekua ni hawaridhishwi na safu yao ya ushambuliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: