Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Yanga wamtangaza Kocha mpya, balaa linaanza upya

Miguel Angel Gamondi Kocha mpya Yanga, Miguel Angel Gamondi

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi kuinoa timu hiyo msimu ujao akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba wake.

Kocha huyo raia wa Argentina ametambulishwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati wa mkutano mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

Gomondi mwenye uzoefu na soka la Afrika kwa zaidi ya miaka 20 amewahi kuzifundisha timu mbalimbali ikiwemo USM Alger ya Algeria, Mamelodi Sundown (Afrika Kusini) na Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kutoa surprise (mshangao) kwa wanachama wake katika mkutano wao kwani Julai mwaka jana ilimtambulisha kiungo wa Burundi, Gael Bigirimana aliyewahi kucheza Newcastle ya England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: