Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Yanga wamtambulisha jezi namba 6 toka Afrika Kusini

IMG 4826.jpeg Skudu Makudubela, Namba 6 wa Yanga

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimya kingi kina mshindo mkuu. Ndivyo ilivyo kwa Klabu ya Yanga baada ya kuzungumzwa kwa muda mrefu mrithi wa namba ya jezi iliyoachwa na Feisal Salum, hatimaye mrithi kawekwa hadharani.

Yanga imemtambulisha skudu Makudubela (33) kutoka Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini ukiwa ni usajili wao mwingine kuelekea msimu mpya 2023/24. Amesaini Mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Marumo Gallants.

Skudu alikuwa akisubiriwa kwa hamu baada ya kuzungumzwa kwa muda mrefu huku sifa zake zikitajwa kwa madaha na Afisa habari wa Yanga.

Skudu anacheza kama winga na ndie anaekwenda kuvaa jezi namba 6 ambayo ina rekodi nzuri kwa misimu kadhaa iliyopita kutokana na aliekuwa anaivaa kufanya vyema na kikosi cha Yanga.

Je ataitendea haki Jezi namba 6? Wananchi kwa Skudu mna maoni gani mmepata au mmepigwa? Tuachie Comment yako

Mtazame vizuri Skudu hapa chini

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: