Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Simba watoa taarifa sakata la Clatous Chama

Chama Complete Clatous Chama

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzungumzwa mengi kwa takribani siku nzima ya leo juu ya mustakabali wa kiungo fundi wa Simba SC Clatous Chama kuwa yuko mbioni kuondoka klabuni hapo.

Sasa Klabu ya Simba kupitia kwa Meneja wa habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally umetoa kauli kuhusiana na sakata hilo.

Ahmed Ally kupitiua ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika;

"Kumekua na sintofahamu kuhusu mkataba wa Mwamba wa Lusaka kiasi cha kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki wetu

Taarifa ni kwamba Chama bado ana mkataba na Simba kwa muda wa mwaka mmoja hadi 2024

Hatujapokea ofa kutoka klabu yeyote ikihitaji kumnunua Chama

Na wala hatujapokea maombi ya mchezaji kutaka kuvunja mkataba

Mchezaji yeyote ambae tunamhitaji atabaki kuitumikia Simba kulingana na mahitaji ya mkataba wetu"

Imesomeka taarifa ya Ahmed Ally, lakini je ina ukweli au tumsubiri na mchezaji atazungumza nini? Tuachie maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: