Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki atangulia AFCON

Aziz Ki Yr Aziz Ki atangulia AFCON

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Tanzania ikilazimika kusubiri hatma yake katika mechi mbili za mwisho kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2023, Stephane Aziz Ki akiwa na timu ya Taifa ya Burkina Faso, wamefuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Ivory Coast mwezi Januari 2024.

Licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Togo juzi, Burkina Faso wamefuzu wakiwa vinara wa kundi B baada ya kufikisha alama 10.

Mali anayocheza mlinda lango Djigui Diarra jana ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Gambia, bado inaongoza kundiĀ  G ikiwa na alama 9.

Fiston Mayele na DR Congo walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mauritania wakati juzi Zambia wanayocheza Kennedy Musonda na Lazarus Kambole walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lesotho na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kufikisha alama 9.

Nyota wote wa Yanga tayari wamekamilisha majukumu yao katika timu za Taifa ambapo baadhi ya wachezaji walijiunga na wenzao Avic Town jana tayari kwa safari ya DR Congo leo Alhamisi.

TIMU saba (7) tayari zimeshafuzu Fainali za AFCON 2023

-Ivory Coast [wenyeji] -Morocco -Algeria -Tunisia -South Africa -Senegal -Burkina Faso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: