Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki aandaliwa kuwamaliza Geita Gold

Aziz Ki 1381 Aziz Ki aandaliwa kuwamaliza Geita Gold

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuukosa mchezo wa jana Jumapili dhidi ya TP Mazembe kutokana na changamoto za usafiri, imefichuka kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki sasa amepewa programu maalum ya kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Geita Gold.

Yanga jana Jumapili walikuwa wageni wa TP Mazembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa nchini DR Congo, huku Aziz Ki akiwa miongoni mwa wachezaji walioukosa mchezo huo wa kukamilisha ratiba kwani tayari Yanga walikuwa wamefuzu Robo fainali.

Jumamosi hii Yanga wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Geita Gold katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumza nasi, Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema: “Aziz Ki alikosekana kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa sababu za changamoto za usafiri lakini alipewa program maalumu za mazoezi kuhakikisha anakuwa fiti kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu wote tunakumbuka mchezo wa mwisho dhidi ya Geita Gold ulivyokuwa na ushindani na sasa tuna vita nyingine ya robo fainali nasi kama mabingwa watetezi ni lazima thakikishe tunashinda na kwenda hatua inayofuata.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: