Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI, Morisson waitanguliza Yanga Fainali Kombe la Shirikisho

Yanga 2  Marumo Gallants Aziz KI, Morisson waitanguliza Yanga Fainali CAF

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC wamebisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, vijana wa kocha Mtunisia, Nasredeen Nabi wakaimaliza Marumo Gallants kipindi cha pili kwa mabao ya viungo marafiki, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Mghana Bernard Morrison dakika ya 90 na ushei.

Sasa Yanga SC wanatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano Mei 17 Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng, NW.

Wakiitoa Marumo, Yanga watakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: