Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam walikamia, Yanga wakacheza kikubwa

Fei Toto Mzez Azam walikamia, Yanga wakacheza kikubwa

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini, Amri Kiemba amesema kuwa katika mchezo wa Nusu Fainali wa Ngao ya Jamii, Klabu ya Azam walipania mchezo huo kama kawaida yao lakini wapinzani wao Yanga SC walicheza kikubwa zaidi na kufanikiwa kuutawala mchezo na kupata mabao.

Yanga jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ndani ya dakika 5 tu na kuamua mchezo huo kwa mabao ya kiungo mshambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.

“Mechi ambavyo ilikuwa kwenye makaratasi, Azam hii ilikuwa inaonekana ya tofauti sana na Azam ya misimu kadhaa iliyopita. Kwenye kila nyakati za usajili, Azam huwa inatarajiwa kuwa tofauti kwa sababu ya namna ambavyo huwa inafanya usajili wake.

“Wakati mechi inaendelea unaona wachezaji wa Yanga walikuwa na jeuri ya wachezaji wa timu kubwa, kulikuwa na tofauti kati ya wachezaji wa Azam na Yanga. Wachezaji wa Azam walionekana wamepania kufanya kitu lakini Yanga walikuwa na mamlaka,” amesema Amri Kiemba.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

MECHI 6 ZA MWISHO Yanga v. Azam

• Yanga SC 2:0 Azam FC • Yanga SC 1:0 Azam FC • Azam FC 2:3 Yanga SC • Yanga SC 2:2 Azam FC • Azam FC 1:2 Yanga SC • Yanga SC 2:0 Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: