Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho, Micho watajwa usajili wa beki kitasa Yanga

Gift X Aucho Micho Aucho, Micho watajwa usajili wa beki kitasa Yanga

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa, kiungo mkabaji wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, Mserbia, Millutin Sredjovic ‘Micho’ wamehusika katika usajili wa beki wa SC Villa ya nchini Uganda, Gift Fred kutua Yanga.

Yanga tayari imefanikiwa kuinasa saini ya beki huyo anayeichezea Timu ya Taifa ya Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba Aucho na Micho wamehusika kwa asilimia kubwa kufanikisha usajili wa beki huyo, baada ya ushawishi mkubwa walioutoa kwa uongozi wa Yanga.

Mtoa taarifa huyo alisema, Micho amehusika kutokana na kufahamu kiwango chake ambaye kila wakati anamuita katika kikosi cha The Cranes.

Aliongeza kuwa, Micho anaamini ujio wa beki huyo kutaimarisha kikosi cha Yanga, wakati wakijiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na uzoefu na uwezo alionao.

“Micho na Aucho wamehusika katika usajili wa Gift, ambao wao ndio waliowathibitishia ubora na kiwango chake ambacho anacho hivi sasa.

“Hiyo ni baada ya kuuliziwa ubora wake na viongozi kabla ya kumpa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga katika msimu ujao ambao tunakwenda kuandika historia nyingine mpya,”

“Hivyo Gift anakuja kupambania namba na mabeki wengine wa kati atakaowakuta hapa Yanga, tunaamini kiwango chake kama uongozi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: