Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafati Haji: Yanga bado hatujamaliza, vyuma vingine vinakuja

Arafat Pic Data Arafati Haji.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema kuwa suala la usajili ndani ya kikosi hichomambo bado unaendelea kwani wanahitaji kuongeza wachezaji wengine kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao 2023/24.

Haji amesema hayo baada ya kusajiliwa kiungo mshambuliaji, Pacome Zouazoua raia wa Ivory Coast na kuongeza kuwa kuna maeneo mawili ndani ya kikosi hicho ambayo yanahitaji kuboreshwa na kuongezewa nguvu, hivyo Wananchi watarajie chuma kingine kutangazwa siku za usoni.

“Tunaona viongozi wanavyopambana kuboresha kikosi na furaha ambayo mashabiki wa Yanga wanaipata kutokana na mafanikio ambayo klabu inayapata.

“Lengo letu msimu huu ilikuwa ni kuhakikisha tunaboresha timu yetu, katika maeneo ambayo yalipendekezwa na mwalimu Nabi aliyeondoka na Gamondi aliyekuja msimu huu.

“Tuna eneo moja ama mawili ambayo bado tunayafanyia kazi ili kuyaongezea nguvu. Usajili tulioukamilisha jana bado sio wa mwisho, hivyo tunaweza kufanya usajili mwingine kabla dirisha halijafungwa,” amesema Arafat haji.

Mpaka sasa Yanga imeshasajili wachezaji watano wa kigeni ambao ni Gift Fred (beki kutoka Sport Villa - Uganda), Maxi Mpia Nzengeli (winga kutoka Maniema – Congo DR), Kouassi Attohoula Yao (beki kutoka ASEC Mimosas), Skudu Makudubela (winga kutoka Marumo Gallants – Afrika Kusini) na Pacôme Zouzoua (kiungo kutoka ASEC – Ivory Coast) wakati wazawa wakiwa wawili, Nickson Kibabage (beki kutoka Singida FG) na Gerard Mkude (kiungo kutoka Simba SC).

Huenda Yanga wakaongeza mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na Kennedy Musonda na kinda Clement Mzize baada ya taarifa kueleza kuwa wameshamuuza mshambuliaji wao kinara, Fiston Kalala Mayele raia wa Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: