Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Tutarudi tukiwa imara zaidi

Ally Kamwe Documentary.jpeg Ally Kamwe.

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amefunguka mara baada ya timu yake kupoteza mchezo wa fainali ya ngao ya jamii baada ya kufungwa na watani zao Simba Sc kwa mikwaju ya penati.

Mchezo huo ulipigwa jana katika Dimba la CCM Mkwakwani ambapo mpaka dakika 90 zinakamilika timu zote zilikuwa hazijafungana ndipo wakaenda kwenye mikwaju ya penati ambapo Simba ilifanikiwa kushinda kwa penati 3-1.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, amesema kuwa wanakiri kupoteza mchezo huo lakini timu yao imeonyesha kiwango bora kuliko wapinzani wao hivyo wana uhakika watarejea wakiwa imara zaidi kwani ndio kwanza msimu unaanza.

"Alhamdulillah, tumepoteza Ngao ya Jamii na ni sehemu ya Football. Tuna season ndefu sana mbele inatusubiri.

"Quality ya Squad yetu imeonekana na mapungufu ya kufanyiwa kazi yameonekana. Ni wakati wa kuelekeza nguvu zetu kwenye Kombe la FA, Ligi Kuu na Champions League.

We will come Back Stronger Wananchi," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: