Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Rais wa Yanga kwenye mkutano mkuu

Hersiiii Yangaaa Eng. Hersi Said

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kutokea Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) ambapo unaendelea Mkutano Mkuu wa Klabu ya Young Africans ambapo Wanachama na Viongozi wamekutana kuzungumza maendelea na mafanikio ya timu yao.

‘Kupitia mfumo wetu wa Wanachama wa matawi katika mwaka 2022/23 tumeweza kukusanya kiasi cha Bilioni 1.3 kama ada ya Uwanachama na Ushabiki kwaajili ya Klabu ya Young Africans’- Rais wa Young Africans, Hersi Said

‘Niwaambie Viongozi wangu kiasi hiki ni kidogo sana ukiangalia gharama za uendeshaji wa CLub Young Africans tulipofika sasa na kama sisi wanachama tutashindwa kuisupport timu yetu financial kuna sehemu Viongozi wenu tutakwama’- Rais wa Young Africans, Hersi Said

‘Na tunakwama sasa hivi tunapata misaada kutoka kwa wadhamini wetu nampigia simu Mheshimiwa Tarimba namueleza nimekwama naomba advance ya miezi mitatu na ananipa lakini pia niwashukuru Azam ambao wamekuwa wakifanya hivyo tunalia saa nyingine timu inahitaji kusafiri mechi mbili za kimataifa mwezi mmoja na wanatusadia na kwa kipekee nimshukuru GSM Ghalib kwa msaada wake mkubwa katika club hii’- Rais wa Young Africans, Hersi Ally  Said

.

‘GSM amekuwa na mchango mkubwa sana wa kufanya mambo mengi ambayo hayapo katika mkataba lakini amekwenda mbali zaidi kutusaidia kupata gharama za kuendesha sehemu ya mahitaji ya timu, tunakushukuru sana Ghalib pamoja na watendaji wake’- Rais wa Young Africans Hersi Ally Said

‘Viongozi tutaendelea kutafuta njia za kuongeza mapato kwa Klabu yetu na pia tunawaomba Wanachama wetu warudi kwenye Matawi yao na kuendelea kuhamasisha kwa nguvu na kuongeza Wanachama na Mashabiki ili kuweza kufikia malengo yetu ya msimu ujao” Rais Hersi Ally Said

‘Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 tumeweza kutengeneza kiasi cha Tsh. 3,550,000,000 kupitia mafanikio yatokanayo na ushiriki wa Klabu yetu katika mashindano mbalimbali” Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said

Aidha Rais wa Yanga SC, Hersi Ally Said katika Mkutano huo Mkuu aliwatangazia Wanachama wake majina mapya ya Wajumbe wa baraza la Wadhamini ambao ni

1.Mama Fatma Karume 2.Mhe. George Mkuchika 3.Mhe. Dr. Mwigulu Nchemba 4.Mhe. Tarimba Abbas 5.Mhe. Anthony Mavunde.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: