Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Albino aliyevalishwa pampasi Simba Day aomba radhi "Mimi ni Yanga"

Fdgf Ali Omari Ali Omary

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia sakata la mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kuonekana kwenye tamasha la Simba Day kitendo ambacho kimetafsiriwa kama ni udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu mhusika afunguka.

Ali Omary ambaye ndiye mhusika ameomba radhi kwa kitendo chake na kubainisha kuwa hakushawishiwa na mtu yeyote kufanya kitendo hicho bali ilikuwa ni njia ya kuonesha ubunifu wake.

"Changamoto nakutana nazo nyingi, nilikwenda kwenye Tamasha la Simba Day na Tunda Man, nikakutana na zari. Na hawa wote ni watu wa Simba Sc.

"Nilikwenda kupiga ndondo, siipendi Simba mimi ni Yanga, Mwananchi wa kutupwa na Simba Day nilikwenda kutafuta pesa, nimewekewa pesa mezani wakaniambia fanya mambo unayoyaweza, nikaenda lakini ndondo haijapendeza.

"Mimi napenda sana kuishi, kucheka na kufurahi na watu, ualbino wangu sitaki kujitia mnyionge, napenda nipambane. Siku za nyuma nilikuwa najiurusha sana nakula sana dawa, nikaamua niache kabisa nimrudie Mungu, nikifanya kwenye ibada ndiyo madili yanakuja.

"Kweli nimefanya vile ninakiri nimekosea, mimi mtoto wao, basi wanisamehe," amesema Ali Omari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: