Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahoua: Nyie nimewasikia subirini kazi

Ahoua Jean Charles Iii Ahoua: Nyie nimewasikia subirini kazi

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulimchukulia poa kiungo mpya wa Simba, Jean Charles Ahoua ulikosea kwani sasa ameanza kuuwasha moto ndani ya mechi mbili tu za Ligi Kuu Bara, na tayari ameahidi kuwa rekodi ndizo zitazungumza.

Ahoua katika msimu wa 2023/24 aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu Ivory Coast (MVP) akiwa na klabu ya Asec Mimosas, huku akifunga mabao 12 na kutoa asisti tisa.

Tangu alipotua nchini amecheza mechi mbili za ligi akiwa na asisti tatu na bao moja huku akishiriki katika mabao mawili kati ya manne iliyofunga Simba dhidi ya Fountain Gate, juzi katika ligi.

“Mabadiliko ndiyo yalinichelewesha kwa kuwa timu ni mpya, lakini kuanzia sasa nataka kuwafurahisha Wanasimba kwa sababu najua kwamba baadhi ya watu walikuwa hawanizungumzi vizuri kwa kuwa nilichelewa kuanza kufunga, lakini haikuwa inaniumiza kwani nilijua tu baada ya muda watanijua mimi ni nani,” alisema juzi.

Kabla ya mechi hiyo, mchezaji huyo kupitia Mwanaspoti alikaririwa baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Tabora United akisema kutoonyesha kiwango kizuri lilikuwa ni suala la muda na hana shaka na kiwango chake.

Hata hivyo, juzi alisema kuwa alihitaji muda wa kuzoeana na wenzake. Alieleza kwamba kilichokuwa kinamsumbua ni mabadiliko ya mara kwa mara kwa wachezaji anaocheza nao eneo la kiungo na hata washambuliaji.

Ahoua anacheza nafasi moja na Agustine Okejepha, Mzamiru Yassin, Debora Mavambo na Kibu Denis, huku akiwa ndiye kiungo pekee aliyetoa asisti nyingi mpaka sasa.

“Simba ina timu na makocha wazuri lakini tunahitaji muda na tunavyoendelea kuwa pamoja kuna kitu kikubwa tunakijenga na baada ya muda mfupi matokeo yataonekana,” alisema.

Aliongeza kuwa,” ninataka kutangulia kwanza kuwatengenezea nafasi washambuliaji kwa kutoa asisti, lakini kama nitapata nafasi nitafunga kwa kuwa najua kufunga.” Simba imesajili wachezaji wengi wa kigeni na wengine kibao imeachana nao, huku ikitarajiwa kuanza mechi za CAF hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: