Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tunarudi kutengeneza Rekodi

Simba Imaraaaa Wachezaji wa Kikosi cha Simba SC wakitoa heshima kwa Mashabiki

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuonekana kama washamaliza msimu wa 2022/23 pasipo kombe lolote, Msemaji wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ametoa ujumbe mzito kwa wapenzi na Mashabiki wa Timu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed ameandika;

Kwa miaka mitano tumekua bora, tumeipa thamani ligi yetu, tumeipa heshima Nchi yetu na tumeiingiza timu yetu kwenye 10 bora za Afrika

Hii haikuja kwa kubahatisha msimu mmoja bali Consistency yetu katika ubora

Ndo maana CAF kwenye vikao vyao wakatuchagua sisi na wengine Saba tukashiriki mashindano makubwa yenye thamani kubwa zaidi Afrika Super League

Mwana Simba huna sababu ya kuwa mnyonge, ili wafikie Level yetu wanatakiwa kufanya hivi kwa miaka mitano ijayo tena kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sio kushindana na timu zinazokaribia kushuka daraja kwenye nchi zao

Tupo msituni tunajipanga upya tuje tutengeneze rekodi yetu barani Afrika

Mnyama hajafa, mnyama anajipanga upya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: