Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Man of the Match ni Ally Salim

Ally Salim Phiri Ahmed Ally: Man of the Match ni Ally Salim

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa katika mchezo wa jana dhidi ya Singida Fountain Gate, man of the match alikuwa kipa Ally Salim kutokana na kuokoa mkwaju wa penati ulioisaidia timu yake kutinga hatua ya Fainali ya Ngao ya Jamii.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya sare ya bao 0-0 huku Simba wakisonga mbele katika hatua ya fainali kwa mikwaju ya penati 4-2 huku Ally Salim akipangua mkwaju mmoja wa Singida na mkwaju mwingine wakipaisha.

"Nina furaha sana kumuona Ally Salim Juma akiendelea kuimarika kwenye eneo la penati, na leo yeye ndio unaweza kumwita Man of the Match.

"Penati ya kwanza aliyookoa dhidi ya Singida Fountain Gate FC ilitupa kujiamini na kuendelea kufanya vizuri kwenye kupiga penati," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: