Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Kila mtu ana kibonde wake wa kumfunga goli 5

Ahmed Ally Viwanja Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Yanga kuanza msimu wa Ligi kwa kutoa kipigo kizito cha mabao 5-0 dhidi ya KMC.

Mashabiki wa Yanga kila mahali wanatembea kifua mbele wakijinasibu kwa ushindi huo mnono na soka tamu la kuvutia.

Sasa katikati ya furaha ya Mashabiki wa Yanga, ameibuka msemaji wa Simba SC Ahmed Ally na kutoa kauli ambayo inaonekana ni kijembe kwenda kwa mtani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed ameandika;

" Kila mtu ana kibonde wake wa kumfunga goli 5"

Kauli hiyo inaonekana kuilenga Yanga ambapo walishawahi kupokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba SC.

Je, Ahmed ally amemaanisha nini? tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: