Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adebayor akaribishwa Simba

ADEBAYOR.jpeg Adebayor akaribishwa Simba

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa RS Berkane ya Morocco, Victorien Adebayor, amekubali kujiunga na klabu ya Simba kwa ajili ya msimu ujao wa ligi baada ya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam.

Adebayor, mwenye umri wa miaka 26, amekubali kujiunga na klabu hiyo, baada kushindikana kujiunga nayo msimu uliopita alipokuwa akiichezea klabu ya US Gendarmerie ya Niger.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa, viongozi wa klabu hiyo walifanya mazungumzo na mchezaji huyo na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili wenye chaguo cha kuongeza mwingine mmoja baadaye.

“Tumezungumzia pia mshahara, bonasi na marupurupu mengine, kifupi asilimia 90 tayari mchezaji huyo atavaa jezi za Simba msimu ujao,” kilisema chanzo kutoka ndani ya klabu ya Simba.

Adebayor alikuwa Tanzania na kikosi chake cha timu ya taifa ya Niger ambacho juzi kilicheza mechi ya kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Hata hivyo kwa sasa mchezaji huyo bado ana mkataba wa klabu ya RS Berkane, na Simba inatakiwa kuongea na klabu yake hiyo kwa ajili ya kumsajili kwani haitompata kama mchezaji huru.

Kwa sasa Adebayor amekuwa hana namba ya kudumu kwenye kikosi cha RS Berkane iliyomsajili mwishoni mwa mwaka jana akitokea US Gendarmerie.

Klabu hiyo iliipiku Simba kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mchezaji huyo ambaye mwenyewe alionekana kuwa na mapenzi na Wekundu wa Msimbazi, lakini mwisho wa siku wakala wake akaamua kumlazimisha kwenda Morocco kutokana na ofa nzuri walioipata.

Simba ilimuona winga huyo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi mwanzoni mwa msimu uliopita na ilikuwa na nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu uliomalizika wa mashindano lakini ilimkosa dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: