Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abdallah Kibadeni aishauri Simba SC 2023/24

Kibaden Abdallah Kibaden

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Mchezaji na Kocha wa zamani wa Simba SC, Abdallah Kibadeni ameutaka uongozi wa klabu hiyo kutofanya makosa katika usajili huku akishauri kutafutwa wachezaji wenye ubora mkubwa kwa ajili ya nafasi ya mabeki wazoefu Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Kibadeni amesema ameangalia kikosi cha Simba SC na kubaini kinahitaji kufanyawa maboresho makubwa na kuwataka viongozi kusajali wachezaji ambao amewapendekeza Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliviera (Robertinho).

Kibadeni amesema amemfuatilia Robertinho kipindi kifupi na kuona mabadiliko ya kikosi cha Simba SC na anaimani viongozi wakimwachia jukumu la kufanya usajili kwa kuleta wachezaji anaowahitaji timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao.

Amesema kulingana na kikosi cha Simba SC kwa sasa wanatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kwa kila nafasi huku akitaka wachezaji watakaosajiliwa wawe na uwezo zaidi.

“Robertinho ni kocha mzuri na viongozi wahakikishe wanafanikiwa kumbakiza mwalimu huyo na usajili watakaofanya lazima wafanye maamuzi magumu kwa kuondoa wachezaji ambao hawana msaada na timu na kusajili nyota ambao wana viwango bora,”

“Wanatakiwa kuanza kuleta mchezaji ambaye anaweza kumpa changamoto yule anayeanza katika kikosi, lazima wasajiliwe wachezaji watakaowezesha Simba kutoka hapa ilipo na kusogea mbele zaidi,” amesema Kibadeni

Ameongeza kuwa Simba SC inacheza michuano mikubwa ya Super League ambayo inashirikisha timu nane bora, wanatakiwa kufanya usajili wenye wachezaji bora ambao watakuwa na hadhi ya kucheza michuano hiyo mikubwa na kufikisha timu hiyo kwenye malengo yao.

Chanzo: Dar24
Related Articles: