Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

A-Z sakata la Chama kutimkia Yanga liko hivi!

Chama Clatous Name Clatous Chota Chama

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za uhakika zilizotufikia ni kuwa Kiungo wa Klabu ya Simba SC, Clatous Chota Chama hana mpango wa kuendelea kusalia ndani ya kikosi hicho na mpaka sasa kuna asilimia 60 raia huyo wa Zambia kuondoka klabuni hapo.

Chama ambaye ni kipenzi cha Wanasimba hajasafiri na kikosi cha Simba SC kilichoondoka nchini juzi kwenda Uturuki kwa ajili ya kambi maandalizi kuelekea msimu mpya.

Chanzo hicho cha karibu na staa huyo kimesema sababu kubwa za Chama kutaka kuondoka Simba SC ni kushindwana katika masuala ya mkataba wa kumfanya kuendelea kusalia mitaa ya Msimbazi.

Aidha, chanzo hicho kimeeleza kuwa, katika Ripoti ya Robert Oliviera "Robertinho" Mwamba wa Lusaka hayupo katika mipango yake kuelekea msimu ujao wa mashindano (2023/2024).

Chama amesema anataka kuondoka Simba SC amepata ofa kutoka timu nyingine na ili abaki anataka aboreshewe maslahi yake, mshahara wake uongezeke kutoka Tsh 14 million kwa mwezi hadi Tsh 30 Milioni.

Chama ameuambia uongozi wa Simba kuwa anahitaji maongezi na ana ofa nzuri mkononi lakini alipoambiwa aseme ofa inatoka wapi amewaambia viongozi jambo hilo ni siri yake.

Thamani ya Chama kwa sasa inaelezwa kuwa imefikia Tsh bilion 2.4 lakini chanzo hicho kimedai kuwa tayari chama amesaini mkataba wa awali na Yanga wenye thamani ya Tsh milioni 671 na mshahara wa Tsh milioni 29 kwa mwezi.

Chanzo kingine kutoka ndani ya Simba kimeeleza kuwa, mkataba wa Chama na Simba umesalia mwaka mmoja (hadi Juni 30, 2023), hivyo Chama anajaribu kutumia mbinu ili kupata mkataba mpya kwa maslahi yake kupitia tetesi za Yanga kumtaka.

Tusubiri mwisho was enema hili utakuwaje?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: