Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibada maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Magufuli yafanyika Chato

Jpm Ibada 12.jpeg Ibada maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Magufuli yafanyika Chato

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ibada maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli, imefanyika katika Kanisa la Mt. Yohana Mria Muzeyi, Parokia ya Mlimani, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, ikiwa ni maadhimisho ya miaka miwili tangu kifo chake kilichotokea tarehe 17 Machi 2021. 

Ibada hiyo imefanyika leo tarehe 17 Machi 2023, kanisani hapo na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi, ambapo familia ya Hayati Magufuli, ikiongozwa na mjane wake, Mama Janeth Magufuli, ilishiriki.



Mbali na familia ya Hayati Magufuli, viongozi wa Serikali walioshiriki ibada hiyo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Zanzibar, upande wa vijana, Mwanaenzi Suluhu Hassan.



Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, katika Hospitali ya Mzena , Makumbusho jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.

Kufuatia kifo chake, aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Rais.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: