Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wajipange, Al Ahli Tripoli ni watu na nusu

Ahli Tripolisisis Simba wajipange, Al Ahli Tripoli ni watu na nusu

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba wanaelekea Libya ???????? kwenye mchezo wao wa kwanza CAFCC msimu huu, wanaenda kukutana na timu yenye ugumu hasa wakiwa kwenye ardhi yao ya nyumbani.

Al Ahly Tripoli kwenye uwanja wao wa nyumbani (Tripoli International Stadium) wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000 tangia February 2023 hawajawahi kupoteza mchezo wowote.

Kwenye kikosi cha Al Ahly Tripoli kuna mchezaji ametokea Esperance de Tunis msimu mwaka juzi Chaalali, huyu mwamba kwenye Transfer Market anavalue ya €900k (Tsh bilioni 2.705) anacheza eneo la Central Midfielder then wana Hamdou El Houni ni left winger ameshawahi kupita timu ya vijana ya Benfica ya Ureno lakini ametokea Wydad Casablanca ya pale Morocco ???????? value yake ni €900k.

Hii miamba ya pale Libya , Al Ahly Tripoli wanammiliki mchezaji mwenye Value ya €1.35 sawa na Tsh bilioni 4.057, mwamba amecheza Petro de Luanda Atletico ya Angola ???????? kabla ya kuelekea De Agosto na baadae İttihad Alex ya Misri: Agostinho Cristóvão Paciẽncia A.K.A Mabululu.

Ni mchezo wa kwenda na tahadhari kubwa, hawa Al Ahly Tripoli wapo vizuri sana wanatakiwa kuingia kwa discipline.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: