Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu bwana hatufai Kinongoni, atupishe - Ndejembi

Asd Ndejembi Mz Huyu bwana hatufai Kinongoni, atupishe - Ndejembi

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kumchukulia hatua za kinidhamu Afisa Ardhi Msaidizi Mwandamizi, Emmanuel Segeja kwa kukosa uadilifu na kuleta taharuki iliyosababisha mgogoro wa ardhi wa viwanja viwili vilivyopo Bahari Beach, Dar es Salaam.

Ndejembi amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi wenye mgogoro alipofika na kusikiliza pande zote mbili na kugundua kuwa Afisa huyo aliruhusu upimaji wa ardhi hizo juu ya upimaji mwingine bila kufuata utaratibu na kupelekea watu kupewa hati miliki nyingine za viwanja hivyo.

“Kwa nini mnafanya vitu bila kujiridhisha kwenye mafaili? Mnatuzulia mgogoro tena ju ya mgogoro tena mwingine why? Unaona shida mliyotusababishia? Yaani mnazua migogoro inaonekana kila siku tunatatua migogoro badala tukae tu’plan’ eeh?

“Miji ipangike, tupime eeh? Katibu Mkuu, huyu bwana huyu hatufai kuwa Kinondoni, kama anaweza akaruhusu vitu hivi vifanyike hatufai kuwa Kinondoni,Siyo tu Kinondoni peke yake, ina maana hatufai kuwa kwenye nafasi aliyo nayo.” Alisema Waziri Ndajembi.

Aidha, Waziri Ndejembi ameelekeza shughuli za ujenzi katika eneo hilo zisimame hadi hapo suluhu ya mgogoro huo itakapopatikana. Katika ziara hiyo Mhe Ndejembi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu, Lucy Kabyemera pamoja na Kamishna wa Ardhi, Mathew Nonge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: