Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy aingilia kati sakata la kichanga kuchungwa ngozi na kukatwa ulimi

Ummy 080903 Facebook Waziri Ummy Mwalimu

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya kufuatilia wamebaini kuna ukweli juu ya taarifa za miili ya Watoto njiti mapacha waliofariki Kituo cha Afya Kaliua kukabidhiwa kwa Wazazi huku Watoto wakiwa wameng'olewa macho, kukatwa ulimi na kuchunwa ngozi kwenye paji la uso.

Waziri Ummy amesema "Tumelifuatilia suala hili, kuna ukweli, Uongozi wa Wilaya ya Kaliua umeshaanza kuchukua hatua, baadhi ya Watumishi wa Afya waliomuhudumia Mama huyu wameshasimamishwa kazi, nakemea vikali kitendo hiki, ninamuagiza RMO Tabora kusimamia vyema Weledi, Maadili na Miiko ya Watumishi wa afya"

Sakata hilo limeibuliwa na Mzazi wa Watoto hao Kisaka Mtoisenga Mkazi wa Ushikola, Kaliua Tabora kupitia kwa Mwanamtandao maarufu na Mdau wa masuala ya Kijamii Malisa @malisa_gj ambaye aliweka malalamiko ya Mzazi huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mzazi huyo amesema baada ya kupewa miili ya Watoto Watumishi wa Afya waliwaambia wakazike haraka kwakuwa Watoto njiti hawafanyiwi msiba na walipofungua box na kubaini miili imenyofolewa macho Watumishi hao wa Kituo cha Afya waliwajibu wakazike tu maana huo ni ushirika na hata walipoenda Polisi na kwa DC wa Kaliua waliambiwa wakazike tu kwakuwa ni ushirikina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: