Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki dunia, wanane wajeruhiwa ajali ya magari manne

Ajali Njombe Z Wawili wafariki dunia, wanane wajeruhiwa ajali ya magari manne

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili ambao majina yao hayajafahamika, wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha zaidi ya magari manne katika eneo la Ichunilo lililopo Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe, Dk Hellen Msesa amethibitisha kupokea miili hiyo na baadhi ya majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo leo Novemba 8,2023.

Amesema saa nne asubuhi wamepokea miili miwili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo pamoja na majeruhi wanane ambapo wanawake ni wawili na wanaume sita.

"Tumepokea majeruhi wanane kati yao wanawake ni wawili wanaume sita na tumepokea waliofariki wawili na wote ni wanaume kwa hiyo jumla yao ni kumi," amesema Msesa.

Amesema kati ya hao majeruhi wawili hali yao siyo nzuri na mmoja amefanyiwa upasuaji na mwingine amepewa rufaa na kupelekwa hospitali ya mkoa.

Amesema miili hiyo haijatambulika lakini ndugu na jamaa wanaendelea kufika hospitalini hapo ili kuweza kuitambua.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Njombe, Bahati Mkutani amesema ajali hiyo imetokea saa tatu asubuhi katika eneo hilo la Kibena barabara kuu ya Njombe kuelekea mkoani Ruvuma.

Amesema baada ya kutokea ajali hiyo walifanya uokoaji kwenye lori lililoanguka lenye shehena ya mzigo wa saruji na baada lori lingine lililobeba mchanga.

"Lori lililobeba mchanga likafeli mfumo wa breki na kuparamia magari takriban manne pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo la uokoaji," amesema Mkutani.

Mmoja ya majeruhi wa ajali hiyo akiwemo Ezekiel Msalilwa wamesema alikuwa kwenye boda boda amepakia abiria kuelekea mjini alipofika eneo la Ichunilo baada ya kuona askari alisimama lakini cha kushangaza kuna gari lilikuja na kumpita upande wa kushoto kwake na kumsukuma kisha kuangukia barabarani.

"Baada ya hapo ndiyo kama hivyo tumeumia tupo hapa kwa ajili ya kupata matibabu na ndiyo tunaendelea na matibabu mpaka sasa," amesema Msalilwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: