Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 14 wa wizi wa kutumia silaha waachiwa

Watuhumiwa 14 Watuhumiwa 14 wa wizi wa kutumia silaha waachiwa

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imewaachia huru watu 14 waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na utakatishaji fedha baada ya kuipitia upya rufaa yao waliyokata kufuatia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Nzega ilipowatia hatiani.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Athuman Matuma alisema mahakama imepitia rufaa za warufani wote na kujiridhisha na ushahidi kadhaa uliowasilishwa na upande Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambao ulikuwa ni maelezo ya onyo kwa washitakiwa yaliyoeleza kukubali kutenda makosa hayo jambo ambalo lilipigwa na warufani hao wakidai kwamba walikubali kwakuwa walipata vipigo na mateso makali ikiwemo kujeruhiwa sehemu za siri na kudhalilishwa.

Jaji Matuma mbele ya warufani hao Mawazo Saliboko na wenzake pamoja na mawakili wao akiwemo Flavia Francis amesema haoni sababu ya kuwatia hatiani kwa ushahidi wa maelezo ya onyo ambayo yalitokana na vitisho na mateso, hivyo amewaachia huru huku tayari wakiwa wameshakaa jela kwa muda usiopungua miaka minane.

Warufani hao walitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Nzega baada ya kupatikana na hatia ya kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha walililodaiwa kulitenda Aprili 21, 2009 ambapo Saliboko na wenzake hao 14 walidaiwa kuvamia Mgodi wa Golden pride wilayani Nzega wakiwa na silaha na kujeruhi walinzi na kupora matofali sita na nusu ya madini ya Dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni nne (4). Uamuzi huo wa Jaji Mfawidhi Athuman Matu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: