Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu watano wafa ajali ya basi Tabora

4 Ajalid Watu watano wafa ajali ya basi Tabora

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu sita wamekufa na wengine 13 wamejeruhiwa wakiwamo watano waliopoteza maisha baada ya basi kugonga lori mkoani Tabora.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Costantine Bugambi alisema ajali ya kwanza ilitokea juzi Mei 21, mwaka huu katika kijiji na kata ya Ilolangulu wilayani Uyui.

Bugambi aliwaeleza waandishi wa habari ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Delux aina ya Tata lenye namba za usajili T 164 DEL likiendeshwa na dereva mwenye umri wa miaka 35 likitoka Kijiji cha Sawewe kwenye Barabara ya Tabora-Urambo.

Alisema basi hilo liligonga lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 584 DTL na kusababisha kifo cha dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Tabora. Dereva wa basi amekamatwa.

Bugambi alisema katika ajali hiyo watu wanne walikufa papohapo na mmoja aliaga dunia wakati anakimbizwa hospitali.

Alisema watu 13 walijeruhiwa katika ajali hiyo na walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Bugambi alisema katika ajali hiyo gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Mamlaka ya Maji Mkoa wa Geita lenye namba za sajili wa STL 9690 liligonga pikipiki yenye namba za usajili MC 483 BVL.

Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 alasiri baada ya mwendesha pikipiki kugeuza ghafla pikipiki akiwa katikati ya barabara eneo la Nkiniziwa wilayani Nzega mkoani humo.

Alisema dereva wa pikipiki alikufa papo hapo na mwili wake uliifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: