Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 6 wadakwa mauaji daktari Tarime

Dk. Isack Daniel G Dk. Isack Daniel Athumani enzi za uhai wake

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Jeshi la Polisi nchini limewadaka watuhumiwa watatu wa mauaji ya Dk. Isack Daniel Athumani aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kerende kilichopo Tarime Rorya mkoani Mara.

Pia limewadaka watuhumiwa wengine watatu waliodaiwa kutekeleza mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) Milembe Selemani. Mtuhumiwa wa nne katika mauaji ya mfanyakazi huyo anadaiwa kujinyonga baada ya wenzie kudakwa.

Taarifa iliyotolewa leo 15 Mei 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema uchunguzi unakamilisha ili watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani.

“Mtakumbuka kuwa Mei 3, 2023 yaliripotiwa mauaji ya Dk. Isack Daniel Athumani ambaye alikuwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Kerende kilichopo Tarime Rorya akitokea kazini.

“Tukio hilo lilifanywa na watu ambao hawakuweza kufahamika kwa mara moja. Jeshi la Polisi lingependa kuwajulisha kuwa watuhumiwa watatu waliofanya mauaji hayo pamoja na kukimbilia Mwanza na baadaye Dar es Salaam wamekamatwa na askari wetu waliobobea katika uchunguzi wa matukio ya mauaji,” amesema na kuongeza

“Mtakumbuka tarehe 26 Aprili 2023 katika mtaa wa Matulole, Kata ya Buhalahala mkoani Geita, kulitokea mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM kwa jina la Milembe Selemani @ Hungwa yaliyofanywa na watu ambao hawakuweza kufahamika kwa wakati huo.

“Kutokana na uchunguzi makini wa askari wanaochunguza matukio ya mauaji, wamefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu na wameonyesha vielelezo walivyotumia katika mauaji hayo pamoja na baadhi ya mali za marehemu, wakati wowote watafikishwa mahakamani,” amesema.

Amefafanya kuwa mtuhumiwa wa nne, baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake na kwamba askari wamefika nyumbani kwake, aliamua kujihukumu mwenyewe kwa kujinyonga.

Amemtaja mtuhumiwa huyo kwa majina ya Pastory Lugodisha @ Buchuchu na alijinyonga tarehe 6 Mei 2023 kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wiayani Sengerema.

Pamoja na mambo mengine amesema Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wahalifu ambao hawataki kuachana na vitendo vya kihalifu ili kufanya kazi halali, watambue kuwa wakifanya uhalifu wowote ule, iwe mchana au usiku ni lazima watakamatwa kwa njia yeyote ile na itakuwa ni aibu kwao na kwa familia zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: