Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili walionyweshwa sumu na baba yao wazikwa Chanika

MAZIKO DGD Watoto wawili walionyweshwa sumu na baba yao wazikwa Chanika

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokea Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, usiku wa jana yamefanyika mazishi ya Watoto wawili Abrahaman Kareem Chamwande na Kauthar Kareem Chamwande, waliofariki dunia baada ya kudaiwa kunyeshwa sumu na Baba yao Mzazi Kareem Chamwande.

Mazishi ya Watoto hao wawili yamefanyika katika makaburi ya Kwa Mwarabu Chanika Mwisho, ambapo inaelezwa Baba wa Watoto hao anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi baada na yeye kutaka kujiua kwa kutumbukia kwenye shimo la choo lakini Polisi ambao waliwahi eneo la tukio kwa kushirikiana na Raia wema walifanikiwa kumuokoa.

Tukio hilo linadaiwa kutendeka usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, huku Wazazi wa Watoto hao Zubeda Ngwale na Chamwande wakiwa wametengana takribani mwaka mmoja uliopita.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wapo katika hatua ya kukamilisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

"Tunamshikilia Kareem ambaye kaua Watoto wake wawili kwa kuwapa juisi yenye sumu na sasa tunashirikiana na Mamlaka zetu za kisayansi kukamilisha uchunguzi huo kwa ajili ya kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa,” amesema Kamanda Muliro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: