Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wadaiwa kujinyonga Mtwara

ACP Isack Mushi ACP Isack Mushi

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linafanya uchunguzi wa matukio mawili ya vifo vya watoto wawili wanaodaiwa kujinyonga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Machi Mosi, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, ACP Isack Mushi amesema kuwa katika tukio la kwanza msichana mwenye umri wa miaka 13 alichukua hatua hiyo baada ya kuzuiwa na kaka yake kwenda kuangalia video usiku kwenye mabanda.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kilomba iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amekutwa amefariki baada ya kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia mtandio wake.

Tukio hilo lilitokea Februari 26, 2023 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Muungano Kata ya Kiromba mkoani humo.

Uchunguzi wa daktari umebaini chanzo cha kifo ni kukosa hewa baada ya kubanwa na mtandio shingoni ambapo uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Mbali na tukio hilo, Kamanda Mushi amesema tukio la pili, mtoto mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Kijiji cha Mnima amekutwa porini akiwa amenyongwa.

Amesema siku ya tukio mtoto huyo alitoka nyumbani na haikujuliakana anakwenda wapi, lakini baadaye mwili wake ulikutwa ukiwa porini ukiwa unaning'inia kwenye mti porini.

Amesema uchunguzi umebaini kuwa marehemu alikuwa anadaiwa Sh8, 000, japo tayari mama yake alikuwa amelipa deni hilo. Kamanda Mushi amesema uchunguzi wa matukio hayo bado unaendelea.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: