Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne mbaroni kwa kuiba mabomba ya mradi wa maji

Jumanne Muliro Dsm Kamanda Muliro

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne eneo la Kibugumo, Kigamboni wakiwa wanaiba mabomba ya mradi wa maji wa Kisarawe II kwenda Kigamboni.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP Muliro Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa tarehe 08/04/2023 maeneo ya Kibugumo, Wilaya ya Kigamboni wakiwa na mabomba aina ya PVC inchi 6 wakiwa na gari yenye namba za usajili T. 719 AGL aina ya Mitsubish Canter.

Aidha SACP Muliro amesema “Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kumkamata dereva wa Canter aliyefahamika kwa jina la Emanuel Msofe mkazi wa Keko Magurumbasi na wenzake watatu wakiwa wanajianda kusafirisha mabomba hayo.”

SACP Muliro ameongeza kuwa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linafanya mahojiano ya kina na watuhumiwa hao ili kubaini kabla ya kuwakamata, wameiba mara ngapi mabomba hayo na mambomba mangapi yameshaiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: