Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wachoma kituo cha polisi, mkuu wa kituo akimbia

Polisi Motooo Wananchi wachoma kituo cha polisi, mkuu wa kituo atokomea

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 28 wanashikiliwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi mkoani humo wakituhumiwa kuvamia na kuchoma Moto Kituo kidogo cha Polisi Kitunda kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 18, 2023 huku Mkuu wa Kituo hicho cha Polisi akikimbia baada ya kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao ameithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza;

“Taarifa ni za kweli na hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa Binadamu. Nipo katika shughuli za Mwenge siwezi kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo.

"Mpaka sasa tunawashikilia watuhumiwa 28, wanaendelea kuhojiwa ili kujua chanzo ya kukichoma moto kituo hicho kidogo na upelelezi unaendelea bado," amesema Kamanda Abwao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: