Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 80 wanusurika kufa bweni likiteketea

Dom 3713211973 Wanafunzi 80 wanusurika kufa bweni likiteketea

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bweni lililokuwa likitumiwa na wanafunzi 80 wa kike katika shule ya Sekondari Doma Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwa vikitumiwa na wanafunzi hao.

Kufuatia moto huo wanafunzi sita wamepata mshtuko na kupelekwa katika Zahanati ya kijiji cha Doma kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na jeshi hilo linaendelea kifanya uchunguzi zaidi.

Mkuu wa Shule hiyo, Edward Laurian amesema unahitajika msaada wa haraka wa kuwawezesha wanafuzi kupata malazi, ambapo hadi sasa baadhi ya wanakijiji wamejitolea kuwapa msaada wa awali.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli amesema serikali itachukua hatua za haraka ili wanafuzi waweze kurejea kwenye hali zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: