Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamuua mama yao kisa imani ya kishirikisha

RPC MUTAFUNGWA WEB 660x400 Wamuua mama yao kisa imani ya kishirikisha

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu sita wa familia moja kwa mauaji ya mama yao mzazi aitwaye Shija Magelanya mwenye umri wa miaka 77 wakimtuhumu kuwaroga wajukuu zake kwa kuwasababisha kupata wendawazimu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe moja ya mwezi huu majira ya usiku ambapo bibi huyo alivamiwa na mwanaume mmoja aliyekuwa na panga kisha akaanza kumkata maeneo ya Kichwani na mabegani na kupelekea kupoteza damu nyingi na kufariki dunia.

Kamanda Mutafungwa amesema watu hao wanashikiliwa kwa mahojiano na pindi uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: