Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa ajali ya New Force Njombe wafikia 7, majeruhi 48

Newforce  180423 InShot Kamanda Imori.

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Makuri Imori amesema idadi ya Watu waliofariki katika ajali ya basi la New Force iliyotokea Mkoani Njombe leo imefikia saba huku majeruhi wakiwa 48.

Basi hilo lenye namba za usajili T173 DZU linalofanya safari zake Dar es salaam - Rukwa lilipata ajali leo baada ya kuanguka wakati liki-overtake lori darajani na kupoteza uelekeo kisha kugonga daraja na kuingia mtaroni katika kijiji cha Igando Kata ya Luduga Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani wa Njombe.

Akizungumza nasi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Makuri Imori, amesema hizo ni taarifa walizonazo hadi wanaondoka eneo la tukio leo ambapo kwa sasa majeruhi wote wapo Hospitali ya Ilembula wakiendelea na matibabu na miili ya marehemu imehifadhiwa pia Hospitalini hapo.

“Mpaka naondoka eneo la tukio majeruhi ni 48 (Wanaume 27 na Wanawake 21) na vifo ni saba (Wanaume watano na Wanawake wawili), nawasihi Madereva waongeze umakini.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: