Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wagawanyika, mgomo Kariakoo

Kariakoo Trs Wafanyabiashara wagawanyika, mgomo Kariakoo

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kusema bado wafanyabiashara wamegawanyika kuhusu kufungua maduka yao. Hii inatokana na baadhi yao kufungua na wengine kutofungua wakisubiria mkutano kati yao na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mwananchi imepiga kambi eneo la Kariakoo kuanzia asubuhi na kubaini kuna baadhi ya wafanyabiashara wamefungua maduka yao huku wengine wakiwa katika vikundi wakijadiliana na kusubiri mrejesho wa kikao cha Waziri Mkuu.

Mmoja wa wafanyabiashara ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema " mimi nimefungua ingawa nasikiliza kikao cha Majaliwa (Waziri Mkuu). Sio kawaida Kariakoo ifike saa moja asubuhi halafu baadhi ya maduka hasa makubwa yasifunguliwe.

"Nadhani wana sababu zao msingi za kutofungua na wapo wengi hawajafungua, nahisi watafungua baada ya kujua kitakachojiri katika kikao cha Waziri Mkuu," amesema mfanyabiashara huyo.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar ea Salaam, Jumanne Muliro ameonekana akiwa na maofisa wake wakitembelea maduka mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.

"Kama ambavyo nimesema jana wafanyabiashara wafungue maduka yao wasiogope, ndio maana tupo hapa kuangalia," amesema Kamanda Muliro aliyeonekana akikatiza mitaa ya Kongo na Tandamti iliyopo katika soko la Kariakoo.

Pia, Mwananchi ilipita katika mitaa mingi ya soko la Kariakoo na kubaini maduka hasa yale yaliyopo katikati mengi hayajafunguliwa huku machinga wakiendelea na biashara kama kawaida.

Pamoja na wamachinga hao kuonekana wamechangamka na kufurahia biashara wengine wameanza ‘kulia’ bidhaa kuwaishia huku wakitaka mgomo huo ufike mwisho.

"Hapa moyoni mwangu natamani hili liishe leo, kesho nitakuwa sina mzigo hivyo nitakuwa sina ninachokifanya tena," amesema Abdurahim Razak ambaye ni mmachinga.

Amesema kwa siku tatu sasa amekuwa na mauzo ya kihistoria ambayo wateja walikuwa wakimuona kama mfalme.

"Unauza bila kukaa, hadi saa saba mchana jana nilikuwa nimeshauza Sh200,000 ni historia," alisema Razak huku akisindikiza na kicheko kuonyesha kufurahia kile anachokifanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: