Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji wa madini wanne wafariki dunia mgodini Mufindi

Mauaji Mgodini Wachimbaji wa madini wanne wafariki dunia mgodini Mufindi

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachimbaji wa Madini wanne wamefariki Dunia huku wengine watatu wakiokolewa baada ya kufikiwa na kifusi katika machimbo ya madini aina ya dhahabu katika Kijiji cha Igomaa, Kata ya Sadani, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana Jumatano, April 19, 2023, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa tukio hilo limetokea April 18 mwaka huu majira 20:39 usiku huko Kijiji cha Igomaa, Kata ya Sadani na Tarafa ya Sadani wilayani hapa katika eneo la machimbo hayo linalomilikiwa na Grece Mgina.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa katika machimbo hao watu saba walifukiwa na kifusi hicho wakiwa wanachimba madini hayo ambapo hadi kufikia Aprili 19, 2023 jumla ya wachimbaji watatu wakiokolewa wakiwa hai huku wengine wanne wakiwa wamefariki Dunia kutokana na kufikiwa na kifusi hicho.

Kamanda ACP Bukumbi amewataja wakiokolewa wakiwa hai katika tukio hilo kuwa Emmanuel Ismail Pengo (36), Abubakari Mohamed Mrangi (33) pamoja na Msafiri Augustino (32) wote wakiwa wachimbaji wa madini na wakazi wa Kijiji cha Igomaa.

"Majeruhi hao baada ya kuokolewa wamekimbizwa katika hospitali ya Mji Mafinga kwa ajili ya Matibabu zaidi ambapo wamelazwa katika hospitali hiyo." Amesema kamanda huyo.

Pia kamanda huyo amewataja waliofariki dunia kuwa Event Tenja Mkazi wa Kilosa Mkoa wa Morogoro, Mathis Mashaka Mkazi wa Kwimba, Mkoa wa Mwanza, Amos Emmanuel Kulwa Mkazi wa Mpigwe Malungwiji pamoja na Nelson Manyusi Mkazi wa Lujewa Mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani hapa limetoa wito kwa wachimbaji wa madini kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za usalama wao hasa kipindi hiki cha mvua nyingi katika uchimbaji huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: