Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh Alhad alaani Kanisa Katoliki kuvamiwa Geita

Hahah Mwenyekiti wa kamati ya amani Sheikh Alhad Mussa Salum

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya amani na maridhiano nchini Tanzania inayojumuisha viongozi wa dini mbalimbali imelaani kitendo cha kuvamiwa kwa kanisa jimbo katoliki la Geita na kufanyika uharibifu wa mali mbalimbali za kanisa hilo.

Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh Alhad Mussa Salum, amesema kamati hiyo imesikitishwa na kitendo hicho ambacho amesema kinapaswa kulaaniwa na watu wote bila kujali dini zao.

Katika hatua nyingine kamati hiyo imeandaa mkutano wa kamati za amani na maridhiano siku ya Ijumaa wiki hii mjini Dodoma utakaofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ambao pamoja na mambo mengine unakwenda kujadili ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto na nafasi ya viongozi wa dini katika kukemea vitendo hivyo.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo mchungaji Christi Sila Kalata kutoka kanisa la KKKT dayosisi ya Mashariki na Pwani amesema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinatokana na mwanadamu kushindwa kumudu tamaa za mwili hivyo viongozi wa dini wanatakiwa kuongeza nguvu kuelimisha waumini wao kutofanya vitendo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: