Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh mil 27 kuchimba kisima baada ya kile cha awali kufukiwa na diwani

Kisima Hgs Sh mil 27 kuchimba kisima baada ya kile cha awali kufukiwa na diwani

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeanza kutekeleza mradi wa kuchimba kisima cha maji kwa ajili ya wananachi wa Kitongoji cha Nyangalamila B kilichoko kijiji cha Nyangalamila Wilaya ya Sengerema baada ya kilichokuwepo kudaiwa kufukiwa kwa amri ya diwani wa eneo hilo.

Tukio la Diwani wa Kata Ilenza, Mneke Mauna kudaiwa kuamuru kufukiwa kwa kisima kilichokuwepo kilipingwa kwa maandamano ya amani ya wakazi wa kitongoji hicho Machi 27, mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine waliiomba Serikali kuwachimbia kisima kingine kuwaondolea adha ya kutumia maji yasiyo salama.

Akizungumza nasi kwa njia ya jana Jumanne Aprili 4, 2023, Mwenyekiti wa Kitongiji cha Nyangalamila B, Fikiri Dotto amesema kilio cha wananchi kimesikika na tayari utekelezaji wa mradi wa kuchimba kisima kirefu eneo hilo unaendelea.

“Tunaishukuru Serikali kwa kusikiliza kilio cha wananchi kwa kuanza kuchimba kisima kirefu katika kitongoji chetu; kisima hiki kitahudumia hadi wananchi wa maeneo jirani,” amesema Dotto

Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Sengerema, George Masawe amesema utekelezaji wa mradi huo umeanza baada ya wataalam wa mamlaka hiyo kujiridhisha na uwepo wa maji ya kutosha chini ya ardhi.

“Zaidi ya Sh27 milioni zitatumika kutekeleza mradi huu ambao siyo tu utatoa maji ya kutosha, bali pia yaliyo safi na salama kwa matumizi yote ya binadamu,” amesema Masawe

Mbunge wa Buchosa kilipo kitongoji cha Nyangalamila B, Eric Shigongo ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo siyo utakaowaondolea wananchi adha ya kutumia muda mwingi kutafuta maji, bali pia matumizi ya maji yasiyo salama.

Mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho, Anastazia John emesema utekelezaji wa mradi huo siyo tu utawaodolea adha kutumia muda mwingi kutafuta maji, bali pia utawapa fursa ya kushiriki shughuli za uzalishaji mali badala ya kuhangaika kutafuta maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: