Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia 6 wa kigeni wafariki kwa ajali Njombe

Ajali Njombe Gs.jpeg Raia 6 wa kigeni wafariki kwa ajali Njombe

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoa wa Njombe wanamsaka dereva na kondakta wa gari aina ya Scania yenye namba za usajili T501 AGJ waliosababisha ajali eneo la Iyai na kupelekea vifo vya watu sita na majeruhi nane wote Raia wa kigeni wakisadikika kuwa ni kutoka Ethiopia.

Akizungumza katika eneo la tukio kamishna msaidizi wa Polisi John Makuri Imori amesema ajali hiyo imetokea mapema alfajiri ya kuamkia hii leo, huku watu sita raia wa kigeni, wakiripotiwa kufariki dunia na wengine nane wakiwa majeruhi, ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya wanging'ombe.

"Ajali hii ilihusisha gari namba T 501 AGJ aina ya Scania iliyokuwa na tela lake lenye namba T595 ANJ iliyokuwa inatoka Makambako kuelekea Zambia baada ya kufika hapa tumekuta ndani ya gari kuna mizigo mingi sana ya vifaa vya ujenzi lakini pia baada ya kufungua tela tumekuta watu ambao ni raia wa kigeni na bahati mbaya hatujapata hati zao zozote za kuwatambulisha," amesema Kmanda Makuri.

Bado raia hao hawajabainika wazi ni kutoka nchi gani, licha ya kwamba taarifa za awali zinabainisha kuwa ni raia wa Ethiopia.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Cloudia Kita ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: