Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mbeya afunguka: ‘Aliye na Esther amuachie’

Himera Mwanafunzi RC Mbeya afunguka: ‘Aliye na Esther amuachie’

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kama kuna Mtu yupo na Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Esther Noah wa Shule ya Sekondari Pandahili aliyepotea May 18, 2023 ni vizuri akamuachia au kama yupo sehemu yoyote ni vizuri Wananchi wakitoa ushirikiano ili apatikane.

Akizungumza kupitia mahojiano na Clouds360 ya @cloudstv leo, Homera amessma kupotea kwa Mtoto huyo ni maumivu makubwa kwa Familia;

“Chukulia Mtoto wako amepotea na hajulikani alipo utajisikiaje?, sisi ni Viongozi lakini ni Wazazi pia tunajisikia maumivu sana na leo tutakuwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ili kujua tumefika hatua gani”

“Pia tutawasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitoa maagizo kwamba huyu Mwanafunzi atafutwe ili ajulikane alipo na alinipigia na kunitumia meseji kwamba baada ya taarifa kukamilika nimtumie taarifa ofisini kwake”

“Jitihada mbalimbali zilifanyika ikiwa na pamoja na kuwahoji Walimu wa Shule, Wanafunzi, Marafiki wa Ester na jumbe zote alizokuwa akiandika zilizoachwa na Mwanafunzi huyo zimechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini kama ni jumbe za Mwanafunzi huyo aliandika mwenyewe au laah!”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: