Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wanne wa familia moja wafa ajalini Lupaso

Ajali Costa Mikumi Mikumi.png Ndugu wanne wa familia moja wafa ajalini Lupaso

Tue, 4 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wa familia moja wilayani Masasi mkoani Mtwara wamefariki papo hapo baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongana na roli aina ya fuso lenye namba za usajili T522 BBQ.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa Masasi Mkomaindo wilayani humo.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu hao wamesema walikuwa wakitokea kumaliza mgogoro wa ndoa yao katika kijiji cha Lufululu na kuelekea Lupaso baada ya kutengana kwa kipindi flani.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkomaindo Masasi, Emmanuel Sabasi amesema kuwa wamewapokea ndugu hao wanne wakiwa wamekufa tayari.

“taratibu nyingine za utambuzi ziliendelea na wote wanne walitambulika. Katika miili hiyo mine kulikuwa na mtoto mdogo wa kiume wa miaka mitano na wengine watatu walikuwa watu wazima. Yupo dada wa miaka 25, na hao wengine wawili mmoja ni miaka 27 na miaka 25.

“Ajali hii imewakuta ndugu hawa wote wanne wa familia moja, hawa watatu wa kiume wamezaliwa na baba wa familia moja, na binti mwingine ameolewa kwenye familia hiyo," amesema daktari huyo.

Taratibu za mazishi zimeendelea baada ya mvutano wa wa ndugu wa marehemu ni wapi miili hiyo ikazikwe baada ya hali ya miili ya marehemu hao kuwa katika hali mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: