Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nauli walituma, tukamteka Air Port - Ahmed Ally

Ahmed Ally Ngoma Sds Nauli walituma, tukamteka AirPort

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba rasmi imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma kwa mkataba wa miaka miwli kwa ajili ya kuimarisha eneo la kiungo la kikosi hicho kwa msimu mpya wa mashindano 2023/2024.

Usajili wa Ngoma umehitimisha kiu ya miaka minne ambayo Simba imekuwa nayo tangu wamtake 2019 akichezea AS Vita ya DR Congo kisha akatimkia Raja Casablanca ya Morocco.

Semaji la CAF, Meneja la habari Simba SC Ahmed Ally akifunguka namna ‘UMAFIA’ ulivyofanyika AirPort.

”Tumewapiga pigo baya mno, pigo la Bruce Lee, tumewaacha wamezungumza na mchezaji wamefika pazuri wakamtumia na nauli.”- Ahmed

Mtoto wa Ally amefunguka ”Simba tukaangalia tukaona Ok, hii ndege inatokaa Ok, itapitia Ethiopia kisha itaingia usiku saa 9 sawa, Paap tukafika AirPort tukawakuta wanamsubiri, yani ni kama vile unasikia mtu kaposa alafu kanyimwa mchumba, ndiyo tulichokifanya wahuni Simba SC.”

”Tumewaangalia wamekaa kizembe, tukamchukua, Ukisia hawaamini macho yao, na mwaka huu watatutambua. Sisi tunachukua tu si ubaya ubaya, yani sisi ni kama Nyoka unamgonga mtu, anakufa na haumlii, ndiyo sisi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: