Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa bodaboda aliyeuawa pamoja na mpenzi wake wazikwa Dodoma

MAUAJI DODOMA M Mauaji ya Dominick Kigula a Esther Shiyago

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa kijana Dominick Kigula (31) aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu yeye pamoja na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake Esther Shiyago (25) umezikwa jana Julai 22, 2022 katika makaburi ya Sechelela yaliyopo kata ya Makulu Dodoma.

Wawili hao waliuawa alfajiri ya Jumatano, Julai 20, 2022 wakiwa kwenye nyumba aliyopanga Dominick mtaa wa Msangalee, kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo anadaiwa kuwa ni kijana mmoja aliyekuwa kwenye mahusiano na Esther na bado anaendelea kusakwa na Jeshi la Polisi.

Marehemu Dominick aliyekuwa akifanya shughuli za kuendesha bodaboda ameacha mtoto wa miaka minne ambaye alikuwa amezaa na mwanamke mwingine aliyewahi kuwa naye hapo awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: