Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa CCM aliyejinyonga azikwa

Mlowo Ccm Mwenyekiti wa CCM aliyejinyonga azikwa

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya Wananchi wamehudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Meshack Mwambogolo huku Familia ikimshukuru Mlinzi wake kwa kufanikisha kuupata mwili wake.

Mwili wa Mwambogolo ulikutwa umening'inia kwenye mti katika msitu uliopo kitongoji cha Iyenga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali huku akiacha ujumbe kwenye gari lake kuwa Familia yake imsamehe kwa maamuzi aliyofanya ya kujinyonga.

Akiongea wakati wa mazishi yaliyofanyika Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali, Mbozi, Msemajo wa Familia ambaye pia ni Kaka wa Marehemu, Williard Mwambogolo amesema kabla ya kwenda kujinyonga alimpa Mlinzi wake Tsh. 10,000.

Msemaji huyo wa Familia amesema baada ya Mlinzi huyo kukaa muda mrefu bila kurudi kutoka kwenye mashamba, Mlinzi huyo alianza kumpigia simu bila kupokelewa “Baada ya muda mlinzi wake alianza kumtafuta usiku kwa kutumia taa ya tochi na kukuta mwili wake umening'inia kwenye mti" amesema

Wakati akitoa taarifa ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya alisema kuwa kabla ya kujinyonga, Mwambogolo alitoa Tsh. milioni 118 na kuziweka kwenye akaunti ya Joseph Muhume kwa ajili ya kununulia kahawa ambapo baada ya kumuingiza fedha hizo Joseph alitoroka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: