Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi aliyejifanya Usalama wa Taifa anaswa Songwe

Augustino Senga Sfd Mwandishi aliyejifanya Usalama wa Taifa anaswa Songwe

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata mwanaume mmoja (jina limehifadhiwa), mwenye miaka 41, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya ofisa usalama wa Taifa.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mwandishi wa habari, inadaiwa kuwa alipita katika mikoa mbalimbali, ukiwemo mkoa huo wa Songwe akijitambulisha kuwa ni ofisa uslama wa Taifa kutoka Ikulu ndogo ya Dar salaam kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wagombea watarajiwa wa nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi wa 2024/ 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jumapili, Mei 5, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amesema mtuhumiwa alikamatwa Aprili 13, 2024 katika Mtaa wa Majengo mapya, wilayani Momba.

Mikoa ambayo mtuhumiwa anadaiwa kupita na kufanya utapeli huo kabla ya kukamatwa mkoani Songwe ni Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: