Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke amuua msanii wa Bongo Fleva kwa kumchoma kisu kisa pesa ya LUKU

Mauaji Arushaaaa Msanii wa Bongo Fleva auawa kwa kuchomwa kisu kisa pesa ya LUKU

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanadada Blandina Fredick Elias mkazi wa Sanawari Juu, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumchoma kisu Erick Adam ambao ni wapangaji wa nyumba moja huku chanzo kikidaiwa kuwa ni fedha ya kununua LUKU ya umeme katika nyumba wanamoishi.

Kwa mujibu wataarifa kutoka eneo la tukio, inadaiwa kuwa baada Blandina kumuomba Erick pesa ya LUKU, ugomvi mkubwa uliibuka jambo lililopelekea Blandina alichukua kisu na kumdunga Erick.

Erick mwenye umri wa miaka 32 anadaiwa kuwa alifariki dunia wakati akiwa njiani akikimbizwa kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu.

Aidha, watu mbalimbali wameumizwa na kitendo hiko huku wakiwaomba wapangaji wapendane kwani watanzania wote ni ndugu hawapaswi kuishi kwa vita kama ambavyo mwanadada Blandina amefanya.

“Majirani wamesema kuwa, kijana huyo alikuwa akijihusisha na shughuli za kuoka mikate katika kiwanda kimoja nchini humo na alikuwa akijishughulisha na Sanaa ya muziki wa Bongo Fleva.

“Tukio limenigusa kwa sababu kijana huyu, sio kwamba ni jirani lakini pia ni mwanafunzi wangu, nimemfundisha shule ya Msingi Luluvani, nilikuwa namfahamu vizuri na alikuwa na akili sana enzi hizo alipokuwa akisoma, nimesikitika sana,” amesema jirani mmoja anayefahamika kwa jina la Benjamin.

Majirani wamesema kuwa suala hilo limewaumiza sana kwani kijana wa watu alikuwa mpole na mwenye kushiriki shughuli za kijamii hata wao wanashangazwa na tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: